NBAA YASISITIZA USHIRIKIANO NA WANAHABARI
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendesha semina maalum kwa wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, ikiwa na lengo la kutoa elimu, kuongeza uelewa na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma katika kuhabarisha jamii kuhusu majukumu ya Bodi hiyo. Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika jijini Dar…