Mwalunenge ataja masoko, kumbi za kisasa akiomba kura
Mbeya. Mgombea ubunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Patrick Mwalunenge ametaja miongoni mwa vipaumbele vyake kuwa ni kuboresha miundombinu ya masoko, kujenga kumbi za kisasa za mikutano na hoteli ya nyota tano ili kubadilisha taswira ya jiji hilo. Amesema atatenga maeneo ya ujenzi wa vibanda vya wajasiriamali wanaopanga bidhaa chini pamoja na…