Dk Tulia aahidi kuanza na vipaumbele 15 Jimbo la Uyole
Mbeya. Mgombea ubunge wa Jimbo jipya la Uyole kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Tulia Ackson, ametaja vipaumbele 15 ambavyo amesema vitabadili taswira ya Uyole ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa halmashauri mpya itakayojitegemea kimapato. Ametoa kauli hiyo jana Jumamosi, Septemba 13, 2025, katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika Shule ya Msingi Hasanga,…