Bado Watatu – 28 | Mwanaspoti
KAMA ningetambua mapema kuwa mauaji yale yalifanywa na mwizi, nisingepata usumbufu wa kuificha ile maiti na kwenda kuitupa. Ningeripoti polisi na nisingepatwa na tatizo lolote.Hapo hapo nikakumbuka kwamba mtu aliyeuawa alikuwa mume wa mtu, na aliuawa nyumbani kwangu usiku wa manane wakati mimi niliyekuwa naye ni mke wa mtu! Je, kama ningeripoti polisi, nini kingetokea?…