Mke wa diwani atokwa chozi la furaha akimnadi mume wake
Mbeya. Mke wa mgombea udiwani Kata ya Ruanda, Lydia Kibonde amejikuta akitokwa chozi la furaha wakati akimnadi mumewe, Isack Mwakubombaki na kutoa shukurani kwa wajumbe na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpitisha kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao. Lydia akizungumza leo Septemba 13, 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa mgombea huyo, amesema anawashukuru…