Samia: Kigoma jiandaeni kuitumia SGR kama fursa ya kiuchumi
Uvinza. Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Kigoma kutumia fursa ya reli ya kisasa (SGR) inayojengwa mkoani humo kwani itakwenda kufungua biashara na uchumi wao. Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa unatekelezwa katika awamu tofauti ili kuunganisha njia kuu za usafirishaji kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma…