Mahakama yabariki faini 30,000 bajaji iliyoegeshwa isivyostahili
Moshi. Ni kama utamaduni wa baadhi ya madereva wa pikipiki za magurudumu matatu maarufu bajaji kuegesha vyombo vyao vya moto popote, lakini bahati haikuwa ya Boniface Mtafya, kwani kosa hilo limemfikisha mahakamani alikotozwa faini ya Sh30, 000. Moshi ni miongoni mwa miji nchini Tanzania, ambayo inakabiliwa na msongamano wa bajaji kutokana na wingi wake kuliko…