Benni McCarthy asiitumie Tanzania kujitetea Kenya
MARA mbili tofauti, Benni McCarthy ameizungumzia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mazingira ambayo hata hakukuwa na sababu za kuitaja au kuizungumzia hadi kijiwe kikamshangaa. Ya kwanza ilikuwa ni baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi ya mashindano ya CHAN 2024 ambapo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari akasema Tanzania iliyokuwa imeongoza…