Takukuru yaonya vitisho, upendeleo na ununuzi wa kura siku ya uchaguzi
Geita. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Geita imewataka wasimamizi wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, kuhakikisha mchakato huo unafanyika katika mazingira salama, yenye haki, bila ununuzi wa kura, vitisho wala upendeleo. Akizungumza leo, Septemba 11, 2025, wakati wa semina ya maofisa uchaguzi ngazi ya jimbo na wasimamizi wasaidizi ngazi…