Mikoa hii kupata mvua pungufu za vuli, tahadhari magonjwa ya milipuko yatolewa
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza utabiri wa msimu wa vuli unaoanza Oktoba hadi Desemba, ikiitaja mikoa saba kupata mvua pungufu. Akitangaza utabiri huo leo Septemba 11, 2025, jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a amesema mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani…