Je, vyuo vikuu vya Tanzania vinaweza kufanya ubunifu kuwa biashara?
Tanzania, kama mataifa mengi yanayoendelea, imewekeza pakubwa katika elimu ya juu kupitia vyuo vikuu vyake. Hivi ni vituo vya maarifa, utafiti na uvumbuzi, vikiwa na jukumu la kuzalisha wataalamu na suluhisho kwa changamoto za jamii. Lakini swali linasalia: Je, ubunifu unaozalishwa unaweza kubadilishwa kuwa fursa za kiuchumi? Kwa muda mrefu, vyuo vikuu vimejikita zaidi katika…