Mgombea udiwani CCM aahidi kukomesha wanafunzi kutembea umbali mrefu

Moshi. Mgombea udiwani wa Kata ya Karanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Deogratius Mallya, ameahidi kushughulikia changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni kwa kuhakikisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata hiyo, akitachaguliwa kuwa diwani. Akizungumza leo, Septemba 28, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika katika kata hiyo, Mallya amesema shule…

Read More

Vyama tisa vyaahidi mabadiliko ndani siku 100 baada ya uchaguzi

Dar es Salaam. Kila kimoja kati ya vyama tisa vya siasa nchini kimetangaza vipaumbele vyake vya utekelezaji ndani ya siku 100 endapo kitapewa ridhaa na wananchi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Miongoni vipaumbele vilivyotajwa na vyama hivyo ni kupatikana kwa Katiba mpya, kudumisha maridhiano ya kitaifa, demokrasia jumuishi, elimu bure kwa ngazi zote…

Read More

Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi ya Sh55 bilioni Rukwa

Rukwa. Mwenge wa Uhuru umepokewa  leo Jumapili Septemba 28, 2025 katika Kijiji cha Kizi, Kata ya Paramawe mkoani Rukwa ambako utakimbizwa kwa kilomita 653.1, huku ukizindua miradi saba ya maendeleo, kuwekea mawe ya msingi miradi 15 na kukagua mingine 12. Shughuli za mapokezi ya Mwenge huo ukitokea mkoani Katavi, zimehudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyombo…

Read More

Wanafunzi Tengeru wang’ara mashindano ya ubunifu ya Afrinnovate Youth Challenge

Arusha. Wanafunzi kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kupitia kikundi chao cha Skyverse Solution, wameibuka washindi wa mashindano ya ujasiriamali na ubunifu ya Afrinnovate Youth Challenge baada ya kubuni mashine ya kubangua karanga. Ubunifu huo umetajwa kuwa mkombozi kwa wakulima wadogo wa karanga, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia nguvu na muda mwingi…

Read More

Chaumma: Tutafuta njaa, tutarudisha tabasamu la Watanzania

Tanga. Mgombea mwenza wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja, ameahidi kurejesha furaha ya Watanzania baada ya kuingia madarakani. Minja amesema kukosekana kwa furaha kunatokana na ugumu wa maisha waliyonayo Watanzania, ikiwemo kupanda kwa bei ya chakula, kodi, ushuru, ukosefu wa ajira pamoja na njaa. Amesema haiwezekani watu wakune vichwa kuhusu kile watakachokula…

Read More

Wavuvi Igombe wapewa elimu ya mpigakura

Mwanza. Wavuvi wa mwalo wa Igombe, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wamepewa elimu ya mpigakura na kuhamasishwa kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili kuchagua viongozi wanaowataka. Elimu hiyo imetolewa leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mwalo huo unaokadiriwa kuwa na wavuvi zaidi ya 5,000. Mvuvi wa mazao ya samaki, Peter Bukanu, amesema elimu aliyoipata…

Read More

Samia aahidi Pwani kuwa kitovu cha usafirishaji, viwanda

Pwani. Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema akipata ridhaa ya miaka mitano mingine Serikali yake itajenga Bandari ya Bagamoyo na kuifanya Pwani kuwa kitovu cha usafirishaji na viwanda nchini. Samia amesema hayo leo Jumapili Septemba 28, 2025 wakati akihutubia mkutano wa kampeni mkoani Pwani katika Uwanja wa Mkuza wilayani Kibaha….

Read More