Watoto wanawatazama na kuwafuatilia kina nani?
Dar es Salaam. Watoto ni vioo vidogo vya jamii. Wanachoona ndicho wanachojifunza, na wanachosikia ndicho wanachojaribu kuiga. Katika zama hizi za mitandao ya kijamii na televisheni, swali kubwa la kujiuliza ni: Watoto wetu wanawatazama na kuwafuatilia kina nani? Je, wanawafuata watu wanaojenga maadili na kuwapa ndoto za maisha bora, au wanawafuata tu wale wanaoonekana maarufu…