Kilanoza ageuza taka za mafuta ya mawese kuwa mkaa mbadala
Kigoma. Mzee Hassan Kilanoza mkazi wa kijiji cha Matiazo, Kata ya Simbo mkoani Kigoma, amekuja na ubunifu wa uzalishaji nishati safi kutokana na fursa aliyoiona. Mzee huyu amebuni mashine maalumu inayozalisha mkaa banifu unaotokana na taka za mabaki ya mafuta ya mawese baada ya kukamuliwa mafuta. …