Kuelekeza kupita kiasi kikwazo kwa mtoto kujifunza
Jumamosi asubuhi, Mariam hupewa jukumu la kufagia sebuleni na mama yake. Kila anaposhika ufagio, mama haishi maagizo. “Anzia pale kona, shika ufagio vizuri, pitisha ufagio kama hivi, usisahau chini ya meza, sasa pindua kiti, hapana, usifagie kwa haraka hivyo. Mtoto wa kike usiwe na haraka unaposafisha nyumba.” Mara nyingine, anapokuwa anaosha vyombo, mama haishiwi maagizo:…