 
        
            Tembo Warriors kupaa kuifuata CECAAF
KOCHA wa timu ya taifa ya Walemavu, Tembo Warriors, Ivo Mapunda amesema timu hiyo itaondoka nchini kesho kwenda Bujumbura, Burundi kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati ya Soka kwa Watu wenye Ulemavu (CECAAF). Mashindano hayo yatakayofanyika kwa siku saba kuanzia Septemba 8-14, yamegawanywa katika makundi mawili. Tembo Warriors ikipangwa Kundi B pamoja na Kenya…
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
         
         
         
         
        