 
        
            Jela miaka 15 kwa kumuua mkewe kwa mchi bila kukusudia
Arusha. Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mtwara, imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela, Shaibu Mtavira, baada ya kumkuta na hatia ya kumuua bila kukusudia mkewe, Aziza Mtelia, kwa kumpiga na mchi kisha kumzika kwenye shamba lao. Shaibu alikiri kumuua mkewe baada ya kutokea kutokuelewana katika mazungumzo yao na kusababisha mapigano kati yao ambapo…
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
         
         
         
         
         
         
        