Upelelezi bado kesi ya polisi kupora bodaboda
Moshi. Jamhuri imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro bado linaendelea na upelelezi wa kesi ya wizi wa pikipiki kwa kutumia silaha inayowakabili askari wanne wa Kitengo cha Intelijensia. Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, Septemba 3, 2025 na mwendesha mashtaka katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali Jackson Matowo, wakati…