Dk Biteko awataka wananchi kutochukulia ‘poa’ uchaguzi mkuu
Geita. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amewataka wananchi kutochukulia ‘poa’ uchaguzi mkuu ujao, bali kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, akisema ni uchaguzi muhimu kwa maendeleo ya nchi. Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Dk Biteko amewataka wananchi kufanya uamuzi…