Mwalimu aahidi utajiri kwa vijana akiingia Ikulu
Tanga. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameahidi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, atahakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa matajiri kupitia njia halali na endelevu. Ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 2, 2025 wakati akihutubia wananchi wa kata za Maramba na Mapatano wilayani…