
Dk Mpango asisitiza elimu ya afya kwa magonjwa yasiyoambukizwa
Dodoma. Serikali imeagiza elimu ya afya kwa Watanzania ianze kutolewa katika ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu ili watu wajue namna bora ya mfumo wa kimaisha. Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Septemba 3, 2025 na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ambaye amesema elimu itasaidia kuwafanya watu wajue namna ya ulaji na vyakula…