
Ahadi ya Mwendokasi Mbagala yakwama tena, sababu zatajwa
Dar es Salaam. Huduma ya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza leo Jumatatu Septemba mosi, 2025, imesogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa miundombinu muhimu yakiwamo mageti janja na kituo cha kujazia gesi. Akizungumza leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 na Mwananchi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart),…