Wawili wauawa Mwanza kwa tuhuma za kuvunja nyumba, wizi wa mali
Mwanza. Watu wawili wamefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa silaha za jadi na wananchi wenye hasira, baada ya kuwatuhumu kuvunja milango na madirisha na kuiba mali za wakazi wa mtaa wa Igelegele, Kata ya Mahina, jijini Mwanza. Waliouawa ni Omary Shaban (24) na Said Bundala (35) waliokuwa wakiishi chumba kimoja cha kupanga katika mtaa huo….