DK.SAMIA:SERIKALI IMESHATUMIA BILIONI 726/- KWA AJILI PEMBEJEO KWA WAKULIMA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi cha miaka minne Serikali imeshatumia Sh.bilioni 726 kwa ajili ya kugawa pembejeo za ruzuku kote nchini. Amesema kuanzia mwaka 2021/22 Serikali ilifanya maamuzi kuanza mfumo wa ruzuku za pembejeo katika zao la korosho na mpaka…