
TLP yaahidi wanafunzi kupanda mabasi bure
Dar es Salaam. Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kikipata ridhaa ya wananchi ya kuongoza nchi miaka mitano ijayo, wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi sekondari watasafiri bure kwenye mabasi. Hatua hiyo imeelezwa ni kutokana na tabu wanayopata wanafunzi wanapokwenda shuleni na wanaporejea nyumbani. Ahadi hiyo imetolewa leo Septemba 4, 2025 na mgombea urais…