Samia awataja wakulima akiahidi kongani za viwanda

Mbalizi.  Leo ikiwa ni siku ya nane tangu kuzinduliwa kwa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 29, 2025, mgombea wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa ahadi kwa wananchi endapo watamchagua. Katika maeneo yote aliyopita, mgombea huyo amekuwa akitoa ahadi zinazolenga kuchochea maendeleo na ustawi wao hasa katika huduma…

Read More

Wadau Afrika Mashariki waungana kukabiliana na uvuvi haramu

Dar es Salaam. Wadau kutoka sekta mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki wameungana kuanzisha juhudi za pamoja za kukabiliana na uvuvi haramu, ambao unaendelea kuwa tishio kwa rasilimali za bahari, mazingira na maisha ya mamilioni ya watu wanaotegemea uvuvi kwa ajili ya kipato na lishe. Hayo yamebainika katika kongamano la Sauti za Buluu lililofanyika hivi…

Read More

Jaji huyu apangiwa kusikiliza kesi ya uhaini ya Lissu

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania sasa iko tayari kuanza usikilizaji wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, baada ya kuipangia tarehe ya usikilizwaji wa awali na jaji atakayeisikiliza. Mmoja wa mawakili wa Lissu, Hekima Mwasipu, amelieleza Mwananchi leo Alhamisi, Septemba 4, 2025 kuwa kesi hiyo…

Read More

Straika Zambia afariki dunia | Mwanaspoti

STRAIKA wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Tapson Kaseba amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu (UTH), baada ya kuugua kwa muda mfupi. Rais wa Shirikisho la soka Zambia, (FAZ) Keith Mweemba ametangaza kifo cha straika huyo akiandika; “Tumesikitishwa na kifo cha Tapson Kaseba tuliyemfahamu kama mchezaji wa zamani…

Read More

Chaumma kubinafsisha sekta ya maji ikishika dola

Dodoma. Mgombea mwenza Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja amesema tatizo la maji nchini litakomeshwa chini ya Serikali ya chama hicho kwa sekta hiyo kubinafsishwa. Amesema ubinafsishaji ni sehemu ya kuondoa kero ya maji ambayo kwa muda mrefu Serikali chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeshindwa kuwapatia huduma ya uhakika Watanzania. Mgombea mwenza…

Read More

Muacheni Yakoub akapambane na Camara

UKIONA mchezaji anasajiliwa na hizi timu zetu mbili kubwa za Kariakoo, yaani Simba na Yanga ukute ana kitu ambacho zimekitathimini na kuona kama kinaweza kusaidia kuimarisha vikosi vyao. Sasa mchezaji kusajiliwa huwa ni jambo moja na kwenda kuipa timu iliyomsajili matunda chanya hubakia kuwa jambo lingine ambalo linaweza kutokea au lisitokee. Kijiweni hapa huwa tunashangaa…

Read More

Mtunzi ajivunia vitabu vyake kusomwa kimataifa kupitia MwanaClick

Dar es Salaam. Ni imani kuwa, mambo yanayohusu vijana yakizungumzwa na vijana wenyewe hueleweka zaidi. Ndivyo anavyoamini Abdulkadir Thabit Massa, hivyo kuwekeza muda wake mwingi kuandika kazi za fasihi zinazohusu vijana. Licha ya kuwapo sera na miongozo inayohusu kundi hilo, bado wenyewe wanapaswa kusimama kueleza wanayokabiliana nayo na kushirikishana fursa na mbinu za kutatua changamoto…

Read More

Henry Joseph ala shavu Fountain Gate

SIKU chache baada ya kocha Denis Kitambi kutua Fountain Gate, amemuongeza kwenye benchi lake la ufundi kiungo wa zamani wa Simba, Henry Joseph. Joseph ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa Moro Kids inayoshiriki First League, ametua Fountain Gate kwa kazi mbili. Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinabainisha kuwa kazi ya kwanza, Joseph amekabidhiwa majukumu ya…

Read More

Teknolojia kuleta mapinduzi ya kilimo

Babati. Wadau wa kilimo nchini watanufaika na teknolojia ya ndege nyuki shambani, ikiwamo kunyunyizia dawa, kupanda mbegu, kupima maeneo na kusafirisha mazao, hivyo kuongeza tija katika kilimo. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za Mati Group, David Mulokozi akizungumza mjini Babati mkoani Manyara, Septemba 4 mwaka 2025 amesema shughuli za kilimo kupitia ndege nyuki zitalenga kuongeza tija,…

Read More