Ulaji maini kupita kiasi watajwa hatari kwa mjamzito

Geita. Maini ni miongoni mwa vyakula vinavyosifika kwa kuwa na virutubisho vingi muhimu, ikiwemo chuma, protini na vitamini A. Hata hivyo, kwa mama mjamzito, ulaji wa maini kupita kiasi unaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto tumboni. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), vitamini A aina ya retinol ikizidi mwilini hasa wakati wa ujauzito,…

Read More

Dk Biteko kuongoza waombolezaji maziko ya Askofu Shao

Moshi. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amewasili katika  Usharika wa Lole Mwika, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuungana na mamia ya waombolezaji katika ibada ya  Maziko ya  Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao (86). Maziko ya Askofu Shao yanafanyika leo, Septemba…

Read More

Wajasiliamali wachangamkia fursa mkutano wa Samia Mbeya

Mbeya. Wananchi na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa mgombea urais wa Chama hicho, Samia Suluhu Hassan. Mgombea huyo ambaye pia ni Rais wa sasa, anatarajia kufanya mikutano minne mkoani hapa baada ya kumaliza ziara yake mkoani Songwe jana Septemba 3, 2025. Kiongozi huyo akiwa mkoani…

Read More

Sababu za kushamiri kwa matumizi kadi za kielektroniki nchini

Miaka michache iliyopita, tulipozungumza kuhusu kadi za malipo, wengi tungefikiri kuwa ni kadi ya plastiki inayotolewa na benki inayotumika kutoa pesa kwenye mashine ya ATM au kupangusa kwenye mashine maalum madukani. Lakini taswira hiyo sasa inabadilika kwa kasi. Ongezeko la matumizi ya simu janja limefanya kadi hizo zisiwe tena kipande cha plastiki kinachoweka mfukoni au…

Read More

Equity kushirikiana na TALEPPA kufufua sekta ya ngozi

Dar es Salaam. Benki ya Equity Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano na Chama cha Watengenezaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA), hatua inayolenga kufungua minyororo ya thamani katika sekta ya ngozi na kuchochea mapinduzi ya kiuchumi kupitia uzalishaji wa viatu vya shule. Makubaliano hayo yameambatana na uzinduzi wa Mradi wa Viatu vya Ngozi vya Shule…

Read More

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 13 jela kwa ufisadi Peru

Rais wa zamani wa Peru, Alejandro Toledo amehukumiwa kifungo cha miaka 13 na miezi minne jela kwa tuhuma za utakatitishaji fedha akiwa madarakani. Toledo (78) anaingia kwenye orodha ya marais wastaafu wengine watano ambao wamehukumiwa kwenda jela kwa tuhuma za ufisadi wakiwa madarakani. Imelezwa kuwa Toledo, aliyekuwa rais kuanzia 2001 hadi 2006, alikutwa na hatia…

Read More

Mkali wa mabao aipa Pamba jeuri

ALIYEKUWA kinara wa mabao wa Kagera Sugar msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara, Peter Lwasa amejiunga na kikosi cha Pamba Jiji ya Mwanza kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji ambalo lilionekana kuwa butu. Lwasa raia wa Uganda alimaliza msimu uliopita akiwa na mabaio manane akishika nafasi ya 11 katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu…

Read More

Simu ilivyofanya mapinduzi ujumuishi wa kifedha Tanzania

Fikiria hali ingekuwaje leo hii kama huduma za fedha kwa njia ya simu zisingekuwepo nchini. Bila shaka unaweza kuvuta picha namna ambavyo kungekuwa na foleni kubwa benki na maeneo mengi ya huduma. Pengine kungekuwa na matukio mengi ya uporaji kutokana na kukithiri kwa matumizi ya pesa taslimu. Suala la kupokea au kutuma fedha kwa ndugu…

Read More