ZEC yaweka wazi watakaopiga kura Zanzibar, 8,325 wakosa sifa
Unguja. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kuwa jumla ya wapiga kura 717,557 ndiyo walioidhinishwa kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, baada ya kukamilika kwa mchakato wa uhakiki wa daftari la kudumu la wapigakura. Akizungumza katika mkutano na wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Jumanne, Septemba 30, 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC,…