
Upatu wa kinamama wasaidia kupata majiko ya nishati safi
Mwanza. Baadhi ya kinamama mkoani Mwanza wameamua kushirikiana kupitia michezo ya upatu ili kumudu gharama za majiko ya nishati safi, baada ya kutambua madhara ya kutumia kuni na mkaa. Kwa muda mrefu, maisha ya kinamama wa Mwanza, hasa wajasiriamali wanaokaanga na kuuza samaki, yamekuwa yakitegemea kuni na mkaa. Hali hiyo si tu imekuwa ikiathiri macho…