Devota Minja: Chaumma italeta unafuu wa maisha kwa Watanzania
Arusha/Katavi. Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devota Minja amesema anasikitishwa na ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania ilhali Taifa limebarikiwa rasilimali nyingi. Akihutubia wananchi wa USA River kwenye mkutano wa kampeni sambamba na kukiombea kura chama chake leo Jumatatu Septemba 22, 2025 Jimbo la Arumeru Mashariki, Minja amesema haiwezekani wananchi…