
Mwili wakutwa kwenye bwawa Kahama
Kahama. Mwanamume ambaye hajafahamika jina wala makazi yake amekutwa amefariki dunia kwenye bwawa la maji lililopo Kata ya Nyihogo, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga. Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Stanley Luhwago akizungumza leo Septemba mosi, 2025, amesema tukio hilo limetokea Agosti 31, 2025. Amesema walipokea taarifa kutoka kwa wananchi waliouona…