Polepole awajibu Polisi baada ya kuitwa ofisi ya DCI
Dar es Salaam. Baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumuita aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kutoa maelezo na ushahidi wa tuhuma alizoibua mtandaoni, yeye amesema ipo nia njema na ovu kwenye wito huo. Kwa mujibu wa Polepole, ipo dhamira njema na ya dhati kwenye wito wa…