Diamond Aahidi Burudani Zaidi kwa Mashabiki Kupitia MSUMARI – Global Publishers




Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa MSUMARI.

Akizungumza mara baada ya kutambulisha ngoma hiyo, Diamond aliwashukuru mashabiki wake kwa mapokezi makubwa na kuahidi kuendelea kuwapa burudani ya kiwango cha juu.

“Nawashukuru sana kwa upendo na mapokezi yenu makubwa kwa wimbo huu. Ni mengi nimewaandalia kuhakikisha mashabiki zangu mnapata raha ambayo sikuwapa kwa muda mrefu 🙏🏽❤️.
#MSUMARI on all platforms now!” – Diamond Platnumz.