DKT NCHIMBI AAHIDI NEEMA NEWALA | CCM KUONGEZA RUZUKU KWENYE MBOLEA NA MBEGU KWA WAKULIMA

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt .Emmanuel John Nchimbi amesema miaka mitano inayokuja Serikali ya Chama hicho imedhamiria kuendelea na mchakato ambao ulianzishwa na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, wa Kuboresha Kilimo ikiwemo pia kuongeza kiwango cha ruzuku ya mbolea kwa Wakulima katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara.Dkt Nchimbi amebainisha hayo leo Oktoba 02, 2025 wakati akihutubia Wananchi kwenye uwanja wa mpira wa sabasaba,

Newala  mjini,kwenye mkutano wake mkubwa wa hadhara wa Kampeni,akiendelea kuzisaka kura za ushindi wa kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Sambamba na hayo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani yake ya Uchaguzi imejielekeza kuboresha Sekta ya Kilimo na Miongoni mwa Vipaumbele vyake ni kuongeza Ruzuku ya Mbegu kwa Wakulima wa hapa Newala na Kanda yote hii ya Kusini, bila kusahau kutanua wigo wa Watalaamu wa Masuala ya Kilimo ‘Maofisa Ugani’, tunataka kuwe na Wataalamu wengi zaidi ili Kilimo Cheti kiwe na Tija” amesema Dkt Nchimbi. 
Awali,Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi ya Chama  Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Samia Suluhu Hassan,pamoja na baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Newala Mjini ,Ndugu Rashid Mohamed Mtima,mgombea Ubunge wa jimbo la Newala Vijijini,Ndugu Yahaya Nawanda pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi anafikisha mkoa wa 16 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,huku akinadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030 kwa Wananchi.