Takriban watu 30 wamefariki dunia na zaidi ya 200 wajeruhiwa baada ya jengo la kanisa kuporomoka nchini Ethiopia. Ajali hiyo imetokea jana Jumatano Oktoba 1, 2025 katika Kanisa la Menjar Shenkora Arerti Mariam lililopo katika eneo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, wakati waumini walipokuwa wamekusanyika kwa ajili ya maadhimisho ya kila mwaka ya kumuenzi Mtakatifu Maria.
Katika taarifa iliyotolewa na Serikali, imetoa pole kwa walioathirika na tukio hilo la kuporomoka jengo na kusisitiza usalama uzingatiwe wakati wa ujenzi.
Mtaalamu wa afya kutoka hospitali ya inayowahudumia majeruhi, Seyoum Altaye, amesema miongoni mwa waathirika ni watoto na wazee na idadi ya vifo huenda ikaongezeka kutokana na watu wengi bado wanaendelea kuokolewa kwenye kifusi.
Baadhi ya watu bado wamekwama chini ya vifusi na juhudi za uokoaji zinaendelea. Majeruhi wengine wamepelekwa katika mji mkuu Addis Ababa kwa ajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, waumini wengi walipanda sehemu ya juu ya kanisa hilo kutazama ujenzi unaendelea muda mfupi kabla ya kuanza maadhimisho ya sherehe ya kumbukizi ya Mtakatifu Mtakatifu wa kanisa hilo