Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wapya katika taasisi zinazohusika na usimamizi wa huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 2, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka, imeeleza kuwa, Said Tunda ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Tunda anachukua nafasi ya Dk Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Aidha, Rais Samia amemteua Pius Ng’ingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), akichukua nafasi ya Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake pia umetenguliwa.