Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali imewataka watumishi wa umma kuzingatia sheria kanuni Taratibu na mienendo ya maadili ya utendaji, na maadili ya taaluma zao, katika utendaji wao wa kazi, ili kutoa huduma bora kwa kuzingatia weledi, uadilifu na uwajibikaji wa hiari kwa lengo la kuimarisha ustawi kwa jamii na kupunguza malalamiko kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Kaimu katibu mkuu wa Ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora Hilda Kabisa leo October 2,2025 katika ufunguzi wa kikao kazi cha sita (6) baina ya ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma na taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaaluma jijini Dodoma.
Kaimu katibu mkuu huyo amesema baadhi ya watumishi wa umma wanatoa lugha zisizofaa, kutojali utu na kitoa majibu yanayokatisha tamaa kwa wateja kinyume na sheria kanuni taratibu mienendo ya maadili ya utendaji na kitaaluma katika utumishi wa umma ambapo amesema mtumishi atakayebainika kufanya hivyo hatua kali za kiutumishi zitachukuliwa dhidi yake.
Hilda ameziasa idara zinazosimamia watumishi kuweka kipaombele kwenye utoaji wa mafunzo ya maadili kwa watumishi wao wapya na waliopo kazini ili utumishi wa umma uwe na watumishi waadilifu wenye mienendo inayoendana na maadili ya taaluma zao na maadili ya kiutumishi ikiwemo kutojihusiha na vitendo vya rushwa.
Amewaasa waajili wote katika utumishi wa umma nchini kuendelea kuwekeza katika utoaji wa huduma bora kupitia matumizi ya mifumo ya kielektroniki iliyosanifiwa na serikali ili kuongeza uwajibikaji uwazi na ufanisi kwa kupunguza mianya na vitendo vya rushwa kwa watumishi katika maeo yao.
Awali akimkaribisha kaimu katibu mkuu huyo, ili kufungua kikao kazi hicho cha sita (6) cha kubalishana uzoefu baina ya ofisi ya Rais menejiment utumishi wa umma na taasisi simamizi za maadili ya kitaaluma, Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora Bi Felister Shuli amesema..
