WALIMU NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA WARAKA NA MIONGOZO YA UTUMISHI WA UMMA

Na Mwandishi wetu Dodoma

 Wakati Kampeni za vyama vya siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu zikiendelea katika mikoa mbalimbali nchini,Tume ya Utumishi wa Umma (TSC) imewstaka walimu kuzingatia walaka na Miongozo ya Utumisho wa Umma juu ya ushiriki wa siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mwenyekiti wa Bodi ya TSC Profesa Masoud Muruke amesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya walimu watakaokiuka maadili.
Amesema Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imeanza maadhimisho ya siku ya Mwalimu duniani ambapo kilele chake kitakuwa  Oktoba 5, mwaka huu jijini humo.
 Pia kuelimisha,kuhamasisha,kuwaenzi na kuwapa motisha katika uwekezaji wa majukumu yao  kuchochea mjadala wa kitaifa na kimataifa kuhusu namna ya kuboresha taaluma ya ualimu na mazingira ya utoaji elimu, 
“Kuchochea mjadala wa kitaifa na kimataifa kuhusu namna ya kuboresha taaluma ya ualimu na mazingira ya utoaji elimu,” alisema
 Alitaja malengo mengine ni kuhamasisha vijana kujiunga na taaluma ya elimu kwa kuona kuwa ni kazi ya heshima na yenye mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii na nchi nzima na kuwa jukwaa la walimu kuelezea maoni yao kuhusu mustakabali wa elimu katika nchi zai na duniani kwa ujumla.
Amesema kuwa maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu ‘Wezesha walimu kuchagua viongozi bora kwa elimu na mafunzo stahiki ‘.