NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
BAADA ya wananchi kulalamika huduma zisizoridhisha katika usafiri wa Mwendokasi hasa kwa wasafiri wa njia ya Kimara, leo Oktoba 2,2025 Serikali imeongeza mabasi mapya na wananchi wameshukuru ujio wa mabasi hayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya abiria wa Kivukoni wameipongeza Serikali kwa kuweza kusikia kilio Chao na kuruhusu mabasi mapya kuingia katika njia ya Kimara.
Alex Michael ambaye ni mtumiaji wa muda mrefu wa mabasi hayo amesema wamekuwa wakikaa muda mrefu vituoni kwa kukosa usafiri wa uhakika kwenye mabasi hayo hivyo kumfanya kutumia gharama kubwa kupanda usafiri mbadala ambao ni bodaboda.
“Baada ya kuanza kwa mradi huu karibu miaka 10, mwanzo huduma ilikuwa nzuri na ilikuwa inavutia sana, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda huduma inakuwa mbovu na mabasi mengi kuharibika”. Amesema Michael