Pichani katikati ni Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wagombea Udiwani katika wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, baada ya kuwahutubia Wananchi katika jimbo hilo la Tandahimba, ambapo baadae alielekea Newala kwa ajili ya kuhitimisha mikutano yake ya Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za CCM, mkoani Mtwara jana Oktoba 02, 2025.
Dkt Nchimbi leo Oktoba 03, 2025, atafanya mikutano miwili ya hadhara akianzia Liwale na kisha kuhitimisha siku kwa mkutano mkubwa wa hadhara katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi.
Dkt Emmanuel Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mikutano yake ya Kampeni za Urais amekuwa akinadi Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030, ambayo imelenga kwa dhati kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuinua hali zao Kiuchumi.