Tunaboresha Usafiri wa Anga Kuongeza Fursa za Utalii Arusha – Global Publishers

Wakazi wa Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, leo Ijumaa Oktoba 3, 2025 wamejitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Wananchi wakiwa na shangwe na nderemo wamesema wamefika kwa hiari yao ili kumsikiliza mgombea huyo ambaye anatarajiwa kunadi ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030 pamoja na sera na ahadi zake kwa Watanzania.

Katika mkutano huo wa hadhara, Rais Samia pia ameendelea kuomba kura za “ndiyo” kwa mafiga matatu yaani Rais, Wabunge na Madiwani, ili kuendeleza utekelezaji wa mipango ya chama hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Baada ya mkutano wa Karatu, Dkt. Samia anatarajiwa kuendelea na kampeni zake ndani ya Mkoa wa Manyara, ambapo maandalizi ya mapokezi makubwa yameelezwa kuwa tayari yanaendelea.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 03, 2025, siku yake ya tatu na ya mwisho mkoani Arusha, katika muendelezo wa kampeni zake za Uchaguzi Mkuu katika Uwanja wa Mnadani, Wilayani Karatu, akisema takribani Shilingi Bilioni 88.5 kujenga kukarabati uwanja wa Lake Manyara kwa kuongeza barabara ya kurukia na kutua ndege pamoja na ujenzi wa jengo la abiria litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia watu 150 kwa wakati mmoja.

Dkt. Samia pia amesema serikali yake itajenga barabara ya kuingia katika kiwanja hicho kwa kiwango cha lami ili kurahisisha shughuli za usafiri na utalii kwa watalii watakaotumia uwanja huo.