ANGELLAH KAIRUKI ASHIRIKI KONGAMANO LA UCHAGUZI, AMANI NA DUA JIJINI DAR ES SALAAM


 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Mhe. Angellah Kairuki, ameshiriki katika Kongamano la
Uchaguzi, Amani na Dua lililoandaliwa na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA)
Wilaya ya Ubungo, Jimbo la Kibamba. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mhe. Kairuki
amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani, huku
akisisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi
wanaowataka kwa hiari na utulivu.

Aidha, amewaomba masheikh na viongozi wa dini kuendelea
kuhimiza amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania kipindi chote cha
uchaguzi.

Mhe. Kairuki pia amewasihi waumini wa Kiislam wa Jimbo la
Kibamba pamoja na Watanzania kwa ujumla kumpigia kura za ndiyo Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumpa
kura nyingi yeye kama Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba, pamoja na madiwani
wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).