Kevin Mbogo Afariki Dunia Baada ya Ajali ya Gari Jijini Dar – Global Publishers



Aliyekuwa mmiliki wa Home Grand Hotels, TCCIA Region Treasurer, na mfadhili wa CCM Wazazi, Kevin Mbogo, amefariki dunia kwa ajali ya gari jana usiku katika eneo la Sayansi, jijini Dar es Salaam.

Marehemu aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Katavi kati ya mwaka 2012 hadi 2017, akiwa na mchango mkubwa katika siasa za vijana na jamii kwa ujumla.

Wadau na marafiki wameshutumika kuomboleza kifo cha Bw. Mbogo, huku mashabiki na wafuasi wake wakimtumia heshima na maombi:

“Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.” 🕊️🕊️