Benki ya Absa Tanzania kuendelea kuwawezesha wajasiriamali wengi zaidi nchini-blogs

 

 

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Mr. Muhammed Shah Newaj (kulia), akizungumza kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya taasisi hiyo na Benki ya Absa Tanzania, wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine’, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.

Mkufunzi wa masuala ya kifedha, Bw. Edmund Munyagi (kulia), akifundisha kuhusu ‘Usimamizi Binafsi wa Fedha’ wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na kuwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, ikishirikisha wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyohusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija ni sehemu ya mikakati ya  Benki ya Absa nchini ya kuwawezesha wajasiriamali sambamba na Lengo la benki hiyo  la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.

Mmoja wa wanawake wajasiariamali mwanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, akichangia hoja wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na usimamizi wa  biashara wenye tija, iliyoandaliwa na taasisi hiyo ikiwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine’, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.

Baadhi ya wanawake wajasiriamali wanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, wakishagilia wakati Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi akizungumza nao wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, iliyoandaliwa na Taasisi ya ASA Microfinance Tanzania kwa uwezeshaji wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine’, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (katikati), baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi  inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na wanachama wao, wakionesha alama ya ushindi mara baada ya semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo  inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.