Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko kali kufuatia kuenea kwa taarifa na mijadala mitandaoni inayolihusisha jeshi hilo na masuala ya kisiasa, likionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa leo jijini Dodoma na msemaji wa JWTZ, Kanali Gaudentius Ilonda, jeshi limesema limeanza kufuatilia kwa karibu watu na kurasa za mitandao ya kijamii zinazojihusisha na kusambaza taarifa zenye lengo la kulichafua au kulipotosha jeshi hilo mbele ya umma.
“JWTZ halijihusishi na siasa. Wajibu wetu ni kulinda mipaka, uhuru na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeona mitandao kadhaa ikijaribu kulitumia jina la jeshi vibaya, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi,” amesema Kanali Ilonda.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.