Said Jr ataja ugumu Malaysia

MSHAMBULIAJI wa Kitanzania, Said Khamis ‘Said Jr’ anayekipiga IFC Malaysia amesema Ligi Kuu ya Malaysia ni miongoni mwa ligi ngumu barani Asia.

Said Jr alikuwepo nje ya uwanja kwa takriban nusu msimu na alijiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Malaysia marufu Liga Super Malaysia akitokea FK Jedinstvo UB ya Serbia aliyoitumikia msimu mmoja mwaka 2023/24.

Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji huyo amesema licha ya kuanza vizuri akifunga mabao matano na asisti moja kwenye mechi sita alizocheza, alikiri ugumu wa ligi hiyo tofauti na ligi alizopita.

“Nimecheza mechi chache lakini ligi ya Malaysia ni ngumu sana inatumia nguvu sana, nimecheza Serbia, Falme za Kiarabu lakini hapa nimepata uzoefu mpya,” amesema Said Jr na kuongeza;

“Tangu nimefika nimekuwa nikipata nafasi ya kuanza na kucheza kwenye kikosi cha kwanza naamini ushindani na wa ligi hiyo umenifanya nipambanie nafasi kwenye timu.”

Said Jr ndiye kinara wa ufungaji kwenye timu hiyo akifunga mabao matano na asiti moja katika mechi sita alizocheza.

Malaysia ni nchi iliyoko Asia ya Kusini Mashariki na ligi hiyo  ni ligi kubwa zaidi nchini humo na timu hushiriki pia michuano ya bara kama vile AFC Champions League na AFC Cup ambayo ni mashindano ya klabu Bara la Asia.

Hii ni mara ya kwanza Said Jr kuitumikia ligi hiyo awali aliwahi kupita Mbao FC kwa msimu mmoja mwaka 2019, kabla ya kusajiliwa na Baniyas iliyokuwa inashiriki Ligi ya Falme za Kiarabu akianzia timu ya