Picha za matukio mbalimbali mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt
Emmanuel John Nchimbi uliofanyika eneo la TASAF, katika Jimbo la Sikonge, mkoani Tabora leo Oktoba 5, 2025.
Katika mkutano huo,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge,Mhandisi Amosy William Maganga na Madiwani.
Dkt. Nchimbi anaendelea kufanya mikutano yake ya hadhara ya kampeni mkoani humo ikiwa ni mkoa wa 18 aliyozunguka kwa ajili ya kumuombea kura Mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea Ubunge na Madiwani.