Vodacom Tanzania PLC imeonyesha kwa mara nyingine dhamira yake ya kuwawezesha wanawake na vijana kupitia michezo kwa kudhamini Ligi ya Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BDL) 2025, ambayo ilihitimishwa kwa fainali zenye msisimko katika kituo cha Don Bosco Oysterbay.
Timu ya DB Lioness imetangazwa mabingwa kwa upande wa wanawake, hatua inayodhihirisha ukuaji wa mpira wa kikapu wa wanawake nchini Tanzania. Ushindi huu ni alama ya nafasi zinazozidi kufunguka kwa wachezaji wanawake na mchango wa Vodacom katika kuendeleza usawa wa kijinsia pamoja na michezo.
Kwa upande wa wanaume, timu ya Dar City Basketball iliibuka mabingwa, huku mchezaji Amini Juma akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Athumani Mlinga. Mchango huu ni sehemu ya mpango mpana wa uwezeshaji vijana unaolenga kukuza vipaji na kuhamasisha kizazi kipya cha wanamichezo nchini.
Tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki, lilihudhuriwa na wafanyakazi wa Vodacom, viongozi wa mpira wa kikapu pamoja na mashabiki wengi, likionesha mshikamano wa michezo na nafasi ya Vodacom kama mdau muhimu katika kukuza mustakabali wa michezo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania Plc, Bw. Athumani Mlinga, akimkabidhi Amini Juma, mchezaji wa Dar City Basketball, hundi ya TZS milioni 10 baada ya timu hiyo kutangazwa mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam (BDL) 2025 kwa upande wa wanaume. Tukio hili lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay, ni sehemu ya mpango wa Vodacom wa kuwainua vijana, kuendeleza mpira wa kikapu na kukuza vipaji vipya nchini Tanzania.
Wachezaji wa DB Lioness wakishangilia baada ya kupokea kombe la ubingwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom, Bw. Athumani Mlinga (wa tatu kushoto). Timu hiyo imetangazwa mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam (BDL) 2025 kwa wanawake, ikionyesha ukuaji wa michezo ya wanawake nchini na jitihada za Vodacom Tanzania PLC kuendeleza vipaji na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo. Tukio lilifanyika mwishoni mwa wiki na kushuhudiwa na wafanyakazi wa Vodacom na viongozi wa ligi.