WASHINDI WA PIKU WAJISHINDIA ZAWADI NONO

Na Mwandishi Wetu

WASHINDI wawili wa promosheni ya Piku Afrika, jukwaa la kidijitali linaloendesha minada ya kipekee mtandaoni, wameeleza furaha yao baada ya kujinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani kubwa kupitia mfumo huo wa mnada wa kidijitali.

Joyce Brown (27), mfanyakazi katika kampuni binafsi, amejishindia simu aina ya Samsung Galaxy A06. 

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Joyce alisema amefahamu kuhusu Piku kupitia rafiki yake ambaye aliwahi kushinda bidhaa mbalimbali kupitia jukwaa hilo.

“Nilipoona rafiki yangu ameshinda zawadi, nilihamasika kujaribu bahati yangu. Kwa kweli Piku ni ya ukweli, hakuna ‘janjajanja’. Nawashauri Watanzania wajitokeze kwa wingi kushiriki, kwani kila mtu ana nafasi ya kushinda,” alisema Joyce kwa furaha.

Naye Witness Saimon (37), mfanyabiashara, amejishindia combo la kike na kiume lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 2. 

Alisema rafiki yake ndiye aliyekuwa akimshawishi kucheza Piku, na baada ya kushawishika, hatimaye ameibuka mshindi.

“Ingawa rafiki yangu bado hajashinda, hajakata tamaa. Anaendelea kushiriki kwa matumaini kuwa siku moja atapata. Napenda kuwapongeza Piku kwa uaminifu wao na namna wanavyowajali washindi wao,” alisema Witness.

Kwa upande wake, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Piku, Barnabas Mbunda, alisema kampuni hiyo inaendelea kutoa fursa nyingi zaidi kwa washiriki wake kupitia minada mbalimbali yenye zawadi kubwa.

Mbunda alisema kuwa, mwisho wa mwaka huu mshindi ataibuka na gari mpya aina ya Toyota Raum, lenye bima ya mwaka mzima na kadi ya mafuta, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.

Pia kutakuwa na mshindi wa mgodi wa Piku atajinyakulia seti ya dhahabu safi yenye thamani ya Sh. milioni 6, na atapata nafasi ya kuchagua mwenyewe dukani seti anayoitaka.

Baada ya siku 28, kupitia Zigo la Piku, mshiriki atakayetoa dau dogo na la kipekee atashinda pikipiki mpya aina ya TVS, ikiwa na helmet, reflector, kadi ya mafuta ya miezi sita na bima, vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 4.

Aliongeza kuwa Kila baada ya siku 14, kwenye Combo la Piku, zitatolewa saa ya kisasa, manukato ya gharama, pamoja na Televisheni ya LG inchi 55 na Airtel Router iliyolipiwa mwaka mzima, zenye jumla ya thamani ya Sh. milioni 2.4.

Mbunda alibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Piku Afrika kupanua wigo wa huduma zake na kuwapa Watanzania nafasi ya kushindania bidhaa kubwa zinazoweza kubadilisha maisha yao.

“Tunawahamasisha vijana na watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea kushiriki. Unachotakiwa kufanya ni kupakua App ya Piku kupitia Play Store kwa watumiaji wa Android au App Store kwa watumiaji wa iPhone,” alisema.

Ameongeza kuwa washiriki wanaweza kununua tiketi kwa bei nafuu kuanzia Sh. 1,000 kwa tiketi 10, Sh. 5,000 kwa tiketi 50, na Sh. 10,000 kwa tiketi 100, huku nafasi ya ushindi ikiongezeka kadri tiketi zinavyoongezeka.