Ahmad Ali awe Kocha Bora wa Mwezi Septemba Ligi Kuu – Global Publishers



Kocha mkuu wa klabu ya JKT Tanzania, Ahmad Ali amechaguliwa kuwa Kocha bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa mwaka 2025/2026 akiwashinda Romain Folz wa Young Africans na Miguel Gamondi wa Singida Black Stars alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za TFF

Ahmad Ali aliiongoza JKT Tanzania kwenye kiwango kizuri katika michezo miwili iliyocheza kwa mwezi huo akiiongoza JKT Tanzania kupata sare ya 1-1 dhidi ya Mashujaa wakiwa ugenini, uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union katika dimba la Mkwakwani, Tanga.